Pata top dress hizi, habari ya mujini kutoka Zenji kwa sh 25,000 rejareja na sh 20,000 jumla. mawasiliano 0715038888







 

Handbag za Scarf Print

    
                              Zilifunga mwaka na bado zinabamba tena mwaka huu, jaribu enjoy!

Una nywele dhaifu? Fanya haya kuzipa uhai..


WANAWAKE wengi hasa wale wanaopenda urembo, huangaika kutunza nywele zao
ili ziwe katika muonekano mzuri, haijalishi ni fupi ama ndefu.

Lakini kwa bahati mbaya, kuna baadhi yao wana nywele dhaifu, na ni wazi kuwa
nywele hizo huwa hazina muonekano mzuri.

Wengi wao wanadhani kuvaa wigi, ama kusuka nywele bandia kwa muda mrefu ni
suluhisho la tatizo hilo, kitu ambacho si kweli kwani nywele hizo zinatakiwa matunzo tu na
kuweka nywele bandia husababisha kuwa dhaifu zaidi.

Kama una nywele dhaifu, basi usipende kupaka rangi za nywele, kwani
kuna baadhi ni kali na hudhoofisha mara dufu, kinachotakiwa ni kufanya stiming
mara kwa mara inayoendana na nywele zako.

Unatakiwa kuwa makini katika kuchagua  mafuta pia, na kama unaona hutoweza
basi mtafute mtaalam wa nywele ili ajaribu kukusaidia kutokana na tatizo lililonalo.





Lishe nayo inahusika, jaribu kula chakula chenye virutubisho sambamba na maji mengi, hii
itakusaidia kwa kiasi kikubwa, lakini pia ni vizuri kama utachagua mafuta
yanayotokana na mimea kwa ajili ya kurutibisha nywele.

Kuweka nywele za bandia kichwani, huzifanya nywele hizo, kukosa hewa na hivyo
kunywea sana na kutofurahia urembo wako.

Kumbuka kuwa muonekano wa mwanamke kwa kiasi kikubwa ni nywele, na uwapo
na nywele asili zenye afya, bila kubandika za bandia, hukufanya kujisikia vizuri na
kuchangia furaha yako ujitazamapo kwenye kioo.

Lipstick ikichanganywa na wanja hudumu muda mrefu!!

Jinsi ya kupaka lipstick na ikakaa muda mrefu mdomoni.

Utafiti wa kiurembo unaonyesha kwamba, upakaji wa lipstick kwa kuchanganya na wanja, husaidia kipodozi hicho kukaa mdomoni kwa muda mrefu mno.

Cha kufanya

Chukua wanja mweusi, anza kwa kuchora mstari kwenye lipsi, kisha changanya wanja mdomo wote, hakikisha haukolei saaana, baada ya hapo chukua lipstick yako paka kwa juu.

Ukimaliza, waweza ongeza na lipbam, lipshine ama vyovyote upendavyo na utakuwa mwakemwake.

Kuchanganya wanja na lipstick husaidia rangi ya lipstick yako kuwa ma giza kidogo na kukaa vizuri mdomoni.




Enjoy!!!!

Faida za asali na mdalasini

Nimeikuta mahali, naibandika kama ilivyo, itusaidie sote jamani!

Imeonekana kuwa asali ukichanganya na mdalasini inatibu maradhi
mengi.Inshallah leo nitaandika kidogo juu ya asali na mdalasini.

Arthritis:
Chukua asali na maji ya dafidafi na uchanganye na mdalasini kidogo
(unga wa mdalasini) changanya uzuri na baadae ujipake sehemu inayouma.
Pia Mwenye ugonjwa huu kila siku asubuhi na usiku atie maji ya moto
(dafidafi) achanganye na vijiko 2 vya meza vya asali na kijiko kimoja
cha unga wa mdalasini anywe kila siku.

Hair loss (utokaji wa nywele):
Kwa wale wote wenye matatizo ya kutoka nywele achukue mafuta ya olive
na ayapashe kidogo achange na kijiko kimoja cha asali, na kijiko
kimoja cha unga wa mdalasini apake katika nywele na awache kwa muda wa
dakika 15 na baadae akoshe.

Toothache (kuumwa na jino):
Changanya kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na vijiko vitano vidogo
vya asali na upake katika jino linalouuma,paka mara 3 kwa siku.

Cholesterol:
Vijiko 2 vya asali na vijiko 3 vya unga wa mdalasini changanya na
ounce 16 ya chai (chai kavu), inapunguza mafuta ndani ya mwili kwa 10&
kwa muda wa masaa 2 tu. Ukinywa kila siku utapunguza mafuta ndani ya
mwili.


Gas:
Changanya asali na mdalasini katika kijiko kikubwa cha meza na unywe.

Ulcers:
Changanya asali na madalasini unywe kila siku.

Heart Disease (Maradhi ya moyo):
Changanya aali na mdalasini na upake katika mkate kuliko kutimia jam
au siagi, na ule kila siku wakati wa chakula cha asubuhi, inapunguza
mafuta katika mishipa ya moyo na inasaidia mtu kupata heart attack,
hata hivo kwa wale waliokuwa washapata heart attack wakitumia hivi
siku zote Inshallah heart attack itaondoka.

Immune Sytem(kujikinga):
Kla siku tumia asali ukicanga na mdalasini inasaidia kuongeza nguvu
katika mwili na inasaidia kuoingeza White blood cells waweze kupigana
na wadudu wa maradhi tofauti.

Pimples:
Vijiko vidogo 3 vya asali na kimoja cha unga wa mdalasini changanya
pamoja na ujipake kwenye pimples usiku wakati wa kulala na asubuhi
ukoshe uso kwa maji ya dafidafi, fanya hivi kwa muda wa wiki mbil
pimples zote huondoka.

Skin Infection(Maradhi ya ngozi):
Cchanganya asali na mdalasini kiwango kimoja na ujipake pia huondoa
ringworms eczema na maradhi yote ya ngozi.

Weith loss (kupunguza uzito):
Kila siku asubuhi kabla kula chakula chochote asubuhi kabla saa
1/2kula chakula cha asubuhi na usiku wakati wa kulala, changanya
asali, mdalasni katika maji ya moto na unywe kila siku hupunguza
mafuta na pia ukiwa unatumia siku zote hata ukila vyakula vya mafuta
basi mafuta hayakai katika mwili.

Cancer:
Kunywa kijiko kimoja cha asali na kijiko kimoja cha mdalasini kwa muda
wa mwezi kila siku mara 3.

Hearing Loss (uziwi):
Kila siku asubuhi na usiku kunywa asali na mdalasini kwa kiwango kimoja.

Bad breath(Harufu mbaya ya kinywa):
Kila siku asubuhi changanya asali na mdalasini aktika maji ya moto na usukutie.

Pole Wema Sepetu kwa kufiwa na baba yako



Blogu hii ambayo ni mdau mkubwa wa masuala ya urembo, inaungana na  mrembo wa nguvu Tanzania, anayetikisa kwa sasa, aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, katika kuombeleza msiba mzito na mkubwa wa baba yake, Balozi Isaac Sepetu aliyefariki dunia leo, tarehe 27, 10, 2013.

Mungu ampe nguvu yeye na familia yake katika kipindi hiki kizito. Inna lilah Waina ilaihi Rajiuun!